Kesi ya mwimbaji wa nyimbo za Injili Emmanuel Mbasha imepigwa kalenda
kwa mara nyingine tena kwa sababu Hakimu anayeendesha kesi hiyo kupata
shughuli nyingine nje ya ofisi.
Mbasha alipanda kizimbani katika mahakama ya Wilaya ya Ilala kwa ajili
ya kusikilizwa kwa kesi yake hiyo ambapo mwendesha mashtaka Kiyoja
Catherine aliahirisha kesi hiyo kutokana na Hakimu Williberforce Luwhego
kupata dharura.
Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa tena 17 October mwaka huu ambapo
Mahakama itaanza kusikiliza ushahidi ambapo upande wa mashtaka utakuwa
na mashahidi wanne kwenye kesi hii inayomkabili mume wa Flora Mbasha
anaekabiliwa na mashtaka mawili ikiwemo ya ubakaji.
Mara ya mwisho kabla ya hii kuahirishwa Flora Mbasha alikwenda
Mahakamani kwa mara ya kwanza akiwa na watu wake na hakukutana wala
kuongea na mume wake ambapo muda mfupi kesi hiyo ikaahirishwa.
No comments: