Muimbaji wa
kike nchini na mmiliki wa Ray Foundation maarufu kama Rayc amethibitisha kuwa
taasisi hiyo imekuwa ikikabiliwa na baadhi ya changamoto ambazozimekuwa
zikiwakwamisha kushindwa kukamilisha mipango waliyo nayo ili kuendeleza taasisi
hiyo inayojihusisha na kuwasaidia vijana ambao ni waathirika wa madawa ya
kulevya .
Akizungumza
na Saut fm jana Ray amesemakuwa miongoni mwa changamoto zinazoikabili taasisi
hiyo ni pamoja na ukosekanaji wa wafadhili kwaajili ya kuwafikia vijana wengi
ambao wamekuwa ni waathirika wa madawa ya kulevya na wanaishi mikoani .
Ray ameongeza
kuwa taasisi yake imefanikiwa kuwasaidia baadhi ya vijana ambao tayari
walikuwa wameathirika na madawa ya kulevya , pia wamekuwa wakijihusisha
na ujasiliamali "Baada mgonjwa kutibiwa na kupona tunampatia ajira
kutokana na fani ambayo anakuwepo nayo, tuna miradi midogo midogo
kwaajili ya kufanya vijana waweze kuwana shughuli za kufanya " Alisema
Rayc






No comments: