headlines

    00:51 A

Slider

BRAND VIDEOS

LAKEZONE MUSIC

WORLD MUSIC

TANZANIA SONG

HOT MIC TV SHOW

GOSPEL

MUSIC

» »Unlabelled » BAADA YA TUKIO LA WIZI WA LAP TOP MSANII LORD EYEZ APIGWA CHINI NA KUNDI LA WEUSI
Unknown


Msemaji kampuni ya Weusi, Nick wa Pili
amesema kuwa rapper Lord Eyez
amesimamishwa na kampuni hiyo
kutokana na kuvunja maadili.

Nick wa Pili amesema baada ya kupokea

taarifa za Lord Eyez kushikiliwa na polisi
huko Arusha kwa wizi wa Laptop walikaa
kikao na kuamua kumsimamisha.
“Kitu ambacho naweza kusema kutoka
Weusi ni kwamba Lord Eyez
tumemsimamisha kazi kikampuni,” Nick
ameiambia Bongo5. “Uamuzi wa
kumsimamisha tumeufikia jana na leo
ndio tumeamua kutangaza rasmi
kwamba Lord Eyez tumemsimamisha
kazi na amesimamishwa kutokana na
misingi na makubaliano ya
kampuni,kulingana na maadili ya
kampuni yetu na mawazo yetu kwa
pamoja ndio yamefanya
tukamsimamisha. Kwahiyo ni kwamba
tumemsimamisha kutokana na
makubaliano ambayo yalifikiwa ndani ya
kampuni ambayo mengine yatabakia
ndani ya kampuni.”

Uamuzi huo wa Weusi umekuja kufuatia

taarifa kuwa Lord Eyez alikamatwa na
polisi kwa tuhuma za wizi wa laptop
Jumamosi, huko Arusha na baadhi ya
picha za tukio hilo kuonekana. Taarifa
hizo zimedai kuwa anatuhumiwa kwa
wizi wa laptop aina ya ‘Dell’.

Mwaka juzi, Lord Eyez alikamatwa na

kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za
wizi wa Power Window za gari la Ommy
Dimpoz, lakini Ommy alitangaza
kumsamehe msanii huyo.

 

«
Next
AUDIO HIT: YOUNG RAFA_FT_DENIS LOVE_FOREVER_PROD BY MNYAMBUDU
»
Previous
YOUNG RAFA NA DOGO D
Pages 22123456 »

No comments:

Leave a Reply